Tupo Nawe

Luc Eymae, msaidizi wake Riedoh Berdien wamalizana na Yanga, Kagera Sugar wajipange

Uongozi wa klabu ya Yanga umeamua kuingia makubaliano na kocha wao mkuu Mbelgiji, Luc Eymae kwa kuingia kandarasi ya mwaka mmoja na nusu ili kuifundisha timu hiyo akichukua mikoba ya Mkongo Mwinyi Zahera.

Luc Eymae alitua nchini wiki iliyopita na kupata bahati ya kuishuhudia timu hiyo ikiwakabili Mtibwa Sugar na kusukumizwa nje kwenye hatua hiyo ya nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup ambayo itafikia tamati yake hii leo usiku.

Mbali na Mbelgiji huyo Yanga pia imemalizana na kocha wao msaidizi Riedoh Berdien kwa mkataba kama huo wa mwaka mmoja na miezi sita ambapo sasa watakuwa wakifanya kazi pamoja na Luc Eymael.

Luc Eymae, kocha msaidizi Riedoh Berdien watashuka dimbani wakianza majukumu yao kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara siku ya Jumatano 15/01/2020 dhidi ya Kagera Sugar.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW