Bongo Movie

Lucy Komba na aliyekuwa mume wa Uwoya waigiza filamu, inaitwa ‘Kwanini Nisimuoe’

Muigizaji mkongwe wa filamu, Lucy Komba anatarajia kuachia filamu iitwayo ‘Kwanini Nisimuoe’ akimshirikisha aliyekuwa mume wa msanii mwenzake Irene Uwoya, Hamad Ndikumana ambapo amedai ni stori ya kweli.

Ndikumana na Lucy Komba
Ndikumana na Lucy Komba

Meneja wa Lucy Komba, Goodluck Komba ambae pia ni kaka wa Lucy, ameiambia Bongo5 kuwa ujio wa kazi hiyo itaufafanua ukaribu wa Lucy na Ndikumana ambao ulizua utata.

“Unajua ukaribu wa Lucy na Ndikumana ulimfanya Irene azungumze vitu vingi kwakuwa alikuwa ni mume wake lakini ukweli ilikuwa ni movie,” amesema Goodluck.

Goodluck amesema kuwa kazi hiyo ambayo Ndikumana ataonekana akila udongo na kujisikia kichefuchefu baada ya mke wake Lucy kushika ujauzito, itatoka Jumatatu huku akiwataka wadau filamu na watanzania kuiunga mkono kazi hiyo yenye stori nzuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents