Habari

Ludacris atoa ofa ya bure kutengeneza jingle za madj

Tulipoisoma tweet ya Ludacris inayosema, “To all the DJ’s that need a drop from me send your scripts to: [email protected] and I got you! #Ludaversal on the way” tulishikwa na butwaa kidogo kwa kutoamini maneno haya!

Lakini huo ndo ukweli! Badala ya kusuburi waandaaji wa show za kimataifa wamlete Ludacris Tanzania ili madj wapate sauti yake, sasa hivi wana uwezo wa kumtumia script wanachotaka aseme na yeye atarekodi na kuwarudishia sauti hizo.

Kwa wasio wataalam wa mambo ya radio ngoja tuwaeleze tweet hiyo ina maana gani. Drops ni zile sauti za wasanii wanaomtaja mtangazaji ama DJ fulani kwenye show yake.

Bila shaka ulishawahi kusikia drops za wasanii kama Keri Hilson, Sean Paul, 50 Cent, Eve na wengine Clouds FM ambao walizirekodi baada ya kuja Tanzania ama kwa mawasiliano maalum!

Maana yake ni kuwa DJ yeyote duniani anaweza kumtumia script Ludacris kwenye email hiyo hapo juu na yeye atairekodi like ‘ This is Ludacris from Atlanta Georgia, I am chilling with the best Dj in Tanzania, DJ blah blah blah only on blah blah blah! Ludaaaaaaaa!” That’s wassup! Madj changamkieni mchongo huo.

Japo madj wengi duniani watamtumia kiasi cha kufanya kazi iwe ngumu kwake kutokana na lundo la script za kuzirekodi, hakuna hasara ukituma na huenda yako ikawa miongoni mwa script zitakazorekodiwa.

Njia hiyo ni moja ya mikakati ya kuitangaza albam yake ya nane Ludaversal itakayotoka miezi ya hivi karibuni.

May 29, 2012 Ludacris aliachia single ya kwanza iitwayo ‘Jingalin’ kutoka kwenye albam hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents