DStv Inogilee!

Ludacris kutumbuiza nchini Ghana Sept. 29

Rapper wa Marekani Ludacris anatarajiwa kuzikonga nyoyo za mashabiki wake nchini Ghana September 29, 2012, kwenye concert kubwa Vodafone 020 Live!

Luda ataperform pamoja na wasanii wengine wakubwa barani Afrika akiwemo Sarkodie wa Ghana, 4×4 na Naeto C wa Nigeria katika jiji la Accra.

Tamasha hilo kubwa kabisa nchini Ghana hufanyika kila mwaka na mwaka huu ni wa tatu tangu lianze.

Kwa upande wao Sarkodie na 4×4 wanatarajia kupiga show yao live kwa kushirikiana na mtayarishaji na mcheza vyombo vya muziki Kwame Yeboah.

Kwame ni producer wa kimataifa ambaye ameshawahi kufanya kazi na wasanii wakongwe kama Stevie Wonder, Cat Stevens, Osibisa, Craig David, Becca, Amakye Dede, Tom Jones na wengine.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW