Habari

LUDEWA: Watakaokaidi kulima zao za biashara kukamatwa na kuswekwa rumande

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, Andrea Tsere ametangaza kuwaswekwa rumande wananchi watakaokaidi kulima zao la biashara.

RC Tsere amesema kutokana na uhamasishaji mkubwa unaoendelea wilayani humo wa kukuza uchumi wa wilaya hiyo ni lazima kila mwananchi wa wilaya hiyo kulima zao la biashara.

Mkuu wa wilaya hiyo amesema hayo jana katika kikao cha hamasa cha wadau/wanaLudewa wanaoishi nje ya wilaya kilichofanyika mjini Njombe, na kutokana na sheria ndogo walizojiwekea ili kuhakikisha kila mtu anakuwa na zao la biashara kwa kuwa wilaya hiyo imekuwa ikikubali mazao mbali mbali ya kibiashara ikiwemo zao la korosho na chai.

Kwa sababu tumeshatunga sheria,mtu yeyote ambaye hatakuwa na shamba la zao la korosho kwenye ukanda wa korosho wote,nimewaambia watendaji hatua ya kwanza tutamkamata tutamuweka Lock up wakati akiwa Lock up tutakuwa tunamuelimisha umuhimu wa kupanda korosho,” amesema DC Adrea Tsere.

RC Tsere amesema sheria kali zitachukuliwa kwa mwananchi ambaye hataweza kushiriki katika mazao hayo.

Tutamshika akielewa akiahidi kwamba atapanda tutamuachia aende kupanda korosho, Lakini kwasababu tumetunga sheria kama ataendelea kuwa mkaidi tutampeleka mahakama ya mwanzo kwasababu kuto kupanda zao la biashara ni ukiukwaji kwa mujibu wa sheria ndogo ya halmashauri.” amesema Andrea Tsere.

Amesema mkuu wa wilaya amepewa mamlaka na Rais kwa mujibu wa sheria ya kumuweka mtu yeyote masaa 24 hakutakuwa na swali lolote ni lazima mkaidi apelekwe rumande kwakuwa ajenda iliyopo kwa sasa ni kujenga uchumi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents