Michezo

Lukaku aiwezesha Ubelgiji kutinga kombe la dunia 2018

Timu ya taifa ya Ubelgiji imekuwa ya kwanza barani Ulaya kufuzu michuano ya kombe la dunia inayotarajiwa kufanyika nchini Urusi mwaka 2018 baada ya kuifunga Ugiriki kwa jumla ya mabao 2-1.

 

Mabao yote matatu ya mchezo huo yamefungwa katika kipindi cha pili ambapo timu ya taifa ya Ubelgiji yakifungwa na Vertonghen dakika ya 70 huku mchezaji Romelu Lukaku akiipatia bao la ushindi dakika ya 74 wakati bao la Ugiriki likifungwa na Rodrigues dakika ya 73 ya mchezo.

Ubelgiji sasa inaongoza kundi H kwa tofauti ya alama nane huku ikiwa imesaliwa na michezo miwili ya kucheza.

Mashetani hao wekundu sasa wanaungana na Brazil, Mexico, Iran na Japan ambao wametinga katika michuano hiyo mikubwa duniani huku Urusi ikiwa imeingia moja kwa moja kama mwenyeji wa michuano hiyo.

Matokeo ya michezo mingine iliyochezwa kufuzu kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018

 

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents