Michezo

Lukaku apigwa faini kwa kusababisha kelele

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ubelgiji, Romelu Lukaku amekubali kulipa kiasi cha dola za kimarekani 450, kwa kosa la kupiga kelele na kuwasumbua majirani zake huko nchini Marekani mwezi Julai, hayo yamesemwa hapo jana siku ya Jumanne na Mahakama kuu ya Jiji la Los Angeles.

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ubelgiji, Romelu Lukaku

Ikiwa ni sehemu ya makubaliano na Idara ya Polisi ya Beverly Hills, Lukaku ameridhia kutoa kiasi hicho cha fedha kama sehemu ya malipo kutokana na kosa hilo na kutokabiliwa na kifungo chochote.

Mshambuliaji huyo wa United mwenye umri wa miaka 24, hakuonekana Mahakamani hapo jana wakati kesi yake ikiendelea.

Tangazo la kukamatwa kwake lilitolewa July 2 baada ya Polisi kupokea malalamiko ya kelele huko Beverly Hills ambako Lukaku alikuwa ameweka makazi yake ya muda akisubiria kutimia kwa dili lake la kujiunga na United ya Ligi Kuu nchini Uingereza akitokea Everton.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents