Michezo

Lukaku atoa ya moyoni “Mourinho amefanya mambo makubwa sana Manchester anahitaji heshima, Ole Gunnar ndio anaanza sasa hivi”

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ubelgiji Romelu Lukaku amefunguka na kutoa ya moyoni yanayomuhusu aliyekuwa kocha wake na klabu ya Man United
Mreno Jose Mourinho.

Mshambuliaji huyo amefunguka na kusema Mourinho anahitaji kupewa heshima yake Manchester United kwa yale aliyoyafanya katika klabu hiyo.

Lukaku amesema “Mourinho amefanya mambo makubwa sana kwa alihitaji heshima yake” Ikumbukwe kwamba Mourinho aliikuta Manchester United wakiwa katika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi lakini aliipandisha hadi nafasi ya pili pia akiwa nafasi ya 6 aliweza kushinda mataji matatu likiwemo la UEFA Europa League.

Akiongea na kituo cha Eleven Sport Lukaku ameongeza:- mourinho alitegemea kujenga kitu kikubwa sana United lakini mambo hayakuenda vizuri naamini kwamba Mourinho amefanya vitu vikubwa sana, alishinda mataji matatu kwa upande wangu namheshimu sana pia ni kocha aliyenisajili mimi”

Lukaku hakuishia hapo maana alimuongelea kocha wake wa sasa hivi Mnorway Ole Gunnar na kusema:-
“Solskjaer ndio anaanza sasa hivi, naamini kila kitu kitaenda vizuri nafikiri tutamaliza ligi katika top four na pia hata kushinda moja ya makombe tunayoshiriki.

Ikumbukwe kwenye UEFA Manchester United watakutana na PSG februari 12 na kwenye FA akipangwa na Chelsea baada ya kutupilia mbali Arsenal ambayo ndio mbabe wa michuano hiyo akitwaa mara 13 na Manchester United mara 12.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents