Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Lukaku aweka rekodi mpya timu ya taifa Ubelgiji

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Manchester United, Romelu Lukaku amefanikiwa kuweka rekodi mpya katika timu ya taifa ya Ubelgiji.

Usiku wa kuamkia Jumatano hii, mchezaji huyo amefanikiwa kufunga goli moja la pekee dhidi ya timu ya taifa ya Japan ambapo limemfanya kufikisha jumla ya idadi ya mabao 31 akiwa na timu ya taifa.

Kwa sasa mchezaji huyo anakuwa ndio mfungaji bora wa wakati wote wa timu hiyo akiwa na umri wa miaka 24.

Lukaku tayari ameshaichezea Ubelgiji mechi 64 mpaka sasa.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW