Michezo

Lukaku na Fellaini kucheza dhidi ya Derby County

By  | 

Kocha wa klabu ya soka ya Manchester United, Jose Mourinho amethibitisha kuwa wachezaji wake Romelu Lukaku na Marouane Fellaini watakuwepo katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Derby County.

Lukaku aliumia katika mchezo dhidi ya Southampton na kulazimika kutolewa nje ya uwanja mapema kipindi cha kwanza wakati Fellaini hajaonekana uwanjani tangu Novemba 2017 kutokana na maumivu ya goti.

“Romelu is okay. From the injured players, Fellaini is back and Michael Carrick is back to training, not competition but he’s back to training with the team. Antonio Valencia will be back to the team next week, but won’t play tomorrow. So the situation is improving for us,” amesema Mourinho.

Kocha huyo ameongeza kuwa katika mchezo huo atamchezesha golikipa wake Romero kwa kuwa ni golikipa bora na De Gea anastahili kupumzika.

Na Raheem Rajuu

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments