Michezo

Luke Shaw ameanza kufanya mazoezi

Mchezaji wa Man United Luke Shaw ambaye ni beki wa kushoto ameanza kufanya mazoezi na wenzake baada ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi saba.

32BE896000000578-0-image-m-108_1459781600537

Mlinzi huyu alivunjika mfupa wa mguu mara mbili katika mchezo wa klabu bingwa ulaya mwezi September walipokua wakicheza na Pvs.

Shaw mwenye umri wa miaka 20 alichezewa rafu mbaya na mlinzi wa Psv, Hector Moreno iliyompelekea kukaa nje ya dimba kwa miezi saba.

Kiungo wa timu ya Man United Juan Mata aliweka picha ya beki huyo akifanya mazoezi na wenzake katika ukurasa wake wa mtandano wa Instagram.

Kwa mujibu wa kocha wa timu ya Taifa ya England, Shaw bado ananafasi ya kuitwa kwenye timu ya taifa itakayoshiriki michuano ya Euro 2016

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents