Uncategorized

Luke Shaw awataka wachezaji kumuheshimu Mourinho ‘Ametupatia mataji matatu ndani ya msimu mmoja, watu wanasahau haraka’

Beki wa Manchester United, Luke Shaw amesema kuwa ni lazima watu wamuheshimu Jose Mourinho kwa kazi aliyofanya ndani ya klabu.

Luke Shaw says Jose Mourinho should be respected for the work he did at Manchester United

Mourinho amekuwa Old Trafford kwa miaka miwili na nasu kabla ya safari yake kuhitimishwa siku ya Jumanne kutokana na matokeo mabovu ya mwanzo wa msimu.

Difenda huyo amesema kuwa siyo vizuri kuonyesha dharau kwa Mreno huyo na anapaswa kuheshimiwa kutokana na mafanikio makubwa aliyoipatia klabu hiyo.

“Siyo kitu kizuri kwa tukio kubwa kama hilo la kutimuliwa Mourinho, nafikiri sisi sote kama wachezaji nilazima tuonyeshe heshima kwa kile kilichotokea,’’ amesema Shaw.

Luke Shaw ameongeza “Watu wanasahau haraka sana kile kilichofanywa na Jose ndani ya United, mataji matatu aliyoshinda, amefanyavingi.’’

“Moja kati ya mataji hayo ni la Europa League ambapo ni moja kati ya makombe hatujashinda hapo kabla, ametupatia mataji matatu kwenye msimu mmoja tu.’’

“Hivyo watu wote wanapaswa kumuheshimu na kukumbuka kile alichofanya, siyo sisi tu bali sote kama timu pamoja na mashabiki kwa pamoja tulishinda mataji yote.’’

Miamba hiyo ya Uingereza ilianza safari mpya mapema wiki hii ikiwa chini ya meneja OleGunnar Solskjaer ambapo hapo juzi siku ya Jumamosi walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5 – 1 dhidi ya Cardiff. Show akiongeza kuwa United ikiwa chini ya meneja yoyote hivyo ndivyo ilipaswa kucheza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents