Habari

Luku yawa tatizo

luku_face

Baada ya watu wa jijini Dar es salaam kuingia kwenye mgao mkubwa wa umeme lakini kuanzia jumatatu hadi leo wamejikuta wakiingia  kwenye zahama lingine la kukosekana kwa vocha za Luku ya umeme baada ya mawasiliano ya mtandao wa luku  kugoma kufanya kazi. Wengi wao wamejikuta wakikesha kutwa nzima


kwenye vituo vya luku na hatmaye wanajikuta wakiondoka bila ya hata umeme kwenye vituo hivyo.  Baadhi ya vituo vilifunga sehemu zao za biashara mapema kwa maana kwamba huduma hiyo kwa siku hiyo haipatikani, lakini vituo vingine vilikuwa wazi huku wateja wakisubiri kwa tumaini la kupata umeme lakini hatmaye mpaka saa tano usiku hakuna chochote kinachoendelea na kuondoka kama walivyokuja.

 

Luku

Kituo hiki cha ‘Manzese chenyewe kiliandika kwa ‘Hakuna Huduma Leo’ kwa maana huduma haitopatikana kwa siku hiyo.

Wengi wa wateja walishauri kama vocha hizo za luku ziweze kuuzwa kama vocha za simu, kwani kufanya hivyo kutapunguza matatizo yasiyokuwa ya lazima kama ilivyokuwa kwa siku mbili hizi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents