Bongo Movie

Lulu aeleza A-Z alivyokuwa na marehemu Kanumba

Muigizaji, Elizabeth Michael (Lulu), amejitetea leo Mahakama Kuu dhidi ya kesi yake inayoendelea Mahakama Kuu ya Tanzania, ambapo leo ameeleza mwanzo mwisho mahusiano yake na marehemu Steven Kanumba.


Lulu akisalimiana na msanii mwenzie wa filamu, Dkt Chein aliyekuwepo Mahakamani hapo.

Mrembo huyo wa filamu anakabiliwa na kesi ya kumuua aliyekuwa mpenzi wake huyo,tukio linalodaiwa kufanyika usiku wa kuamkia tarehe 7 mwezi Aprili mwaka 2012.

Lulu amejitete hivi Mahakamani hapo: Nilipofika kwa marehemu Kanumba nilimkuta yupo kwenye dressing table, nilikaa kitandani kwa kuwa hapa kuwa na sehemu ya kukaa.

Nilikuwa nataka kutoka na marafiki zangu ila marehemu alinikataza, alikuwa hataki nitoke, nilipomwambia natoka na marafiki zangu akaniambia nipitie nyumbani kwake nikamuage, hivyo nikaenda mpaka nyumbani kwake kumuaga.

Baada ya kufika pale simu yangu iliita akadhani naongea na mwanaume akaniuliza unaongea na mwanaume mbele yangu? Akaanza kunipiga na mara nyingi alikuwa akinipiga alikuwa ananipiga akiwa amelewa na sio kwa akili zake.Pia akilewa anakuwa haogopi mtu yoyote yule ila akiwa hajalewa anaogopa publicity kwasababu alikuwa hapendi,” amesema Lulu.

Alivyoanza kunipiga nikataka kukimbia akawa ananikimbiza na taulo huku akiwa peku na mimi nilikuwa naogopa kupigwa, huku akiwa na panga lake alilolitoa uvunguni mwa kitanda,” ameeleza Lulu.

Marehemu alianguka mwenyewe na kujigonga kwa nguvu na kuinuka akitapatapa, nilimwambia Seth kuwa Kanumba amedondoka na akajaribu kumuamsha hakuamka, akasema anaenda kumuita daktari, alivyosema anaenda kumuita daktari na mimi nikaondoka nikiogopa anaweza akaamka akaanza kunipiga. Niliondoka nikawasha gari kuelekea Coco Beach kutuliza akili”.

“Nilivyofika Coco Beach meseji zilianza kusambaa kuniuliza kuwa nasikia Kanumba amefariki, nikampigia Kidume ambaye ni rafiki yake Kanumba kumuuliza Kanumba yupo hospitali gani niende kumuona, akaniambia wewe usije hospitali, niambie uko wapi, tukakubaliana tuonane Bamaga. Tulivyokutana Bamaga alikuwa kama anataka kuongea na mimi ghafla wakaja askari kunikamata.

“Na kunipeleka Oysterbay polisi, nilipofika Oysterbay nilikuta watu wengi sana niliyemtambua ni Ray. Nilijua Kanumba amefariki nikiwa polisi. Nilipomkuta Ray Oysterbay polisi nikajua Kanumba amekamatwa kwa sababu ya makelele niliyokuwa nayapiga kule nikajua watu walisikia.Kwa namna yoyote ile mimi sijasababisha kifo cha Kanumba, na mimi ndiye nilieshambuliwa na marehemu.”

Kwa upande Daktari bingwa wa uchunguzi wa magonjwa ya binadamu, Innocent Mosha kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili ameieleza Mahakama Kuu alichobaini baada ya kuufanyia uchunguzi mwili wa msanii wa fani ya uigizaji wa filamu nchini, Steven Kanumba aligundua ubongo wa Marehemu ulitikisika na mishipa kujaa damu.

Dk Mosha ambaye ni shahidi wa nne wa upande wa mashtaka katika kesi ya kuua bila ya kukusudia inayomkabili msanii wa filamu nchini ,Elizabeth Michael(Lulu) aligundua ubongo wa Marehemu ulitikisika na mishipa kujaa damu.

Dkt Inocent amesema alikabidhiwa maiti ya kanumba aifanyie uchunguzi hospitali ya Taifa Muhimbili aligundua ubongo wa Marehemu ulitikisika na mishipa kujaa damu kupelekea kukosa Hewa hadi mauti kumpata.

Alieleza kuwa lakini tatizo hilo linaweza kusababishwa na kujigonga ukutani au kugongwa au kupigwa na kitu, huku alieleza kuwa walimfungua tumboni hakukua na tatizo ila mapafu yalijaa damu na alitoa kipande cha ini na figo na mkojo kupeleka kwa Mkemia Mkuu.

Jaji kasema kutokana na ushahidi huo mshtkiwa anayo kesi ya kujibu ambapo wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala kaimbia Mahakama mshtkiwa amejitetea mwenyewe leo hii.

Kesi inaendelea kesho tarehe 24, Oktoba mwaka huu ambapo upande wa utetezi kujitetea na anaekuja kujitetea kesho ni Josephine Mushumbusi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents