Aisee DSTV!

Lulu ajipanga kuja na filamu ya comedy (Picha)

Msanii wa filamu Elizabeth Michael aka Lulu anatarajia kuja kivingine na filamu mpya ya comedy.

df
Lulu akiwa location

Akizungumza na Bongo5 jana kwenye uzinduzi wa filamu mpya ya ‘Mpango Mbaya’ iliyo chini Proin Promotions, mwenyekiti wa kampuni hiyo Johnson Lukaza alisema wameamua kumpeleka Lulu katika upande wa serious comedy.

“Filamu ipo kwenye process,” alisema Lukaza. “Wapo kwenye shooting na soon itatoka filamu ya Lulu ambayo ataonekana anakuja kivingine kabisa kuliko walivyomzoea. Lulu atachekesha sana yaani anakuja na serious comedy, atacheza character zote kuonyesha uwezo wake wa sanaa na kuonyesha umahiri,” aliongeza.

Katika hatua nyingine Lukaza amezungumzia mapokezi ya filamu ya ‘Mpango Mbaya’ inayowashirikisha wasanii walioibuliwa kwenye shindano la Tanzania Movie Talent 2014 (TMT) baada kuzinduliwa na kuangaliwa kwa mara ya kwanza katika jumba la sinema Mlimani City.

IMG_0291
Mwanaafa Mwinzago mshindi wa mshindi wa TMT mwaka 2014, ndiye mhusika mkuu wa filamu ya Mpango Mbaya

“Hatua ya kwanza ilikuwa ni kutafuta vipaji halisi na kuwapatia elimu ya uigizaji. Kupitia TMT na hatua ya pili ni kuwachanganya na wasanii waliopo katika tasnia pili ni kwenda kimataifa kwa filamu yao ya Mpango Mbaya kurushwa katika jumba la sinema,” alisema Lukaza.

Tazama picha za uzinduzi wa filamu hiyo.

Baadhi ya wahusika wa filamu hiyo
Baadhi ya wahusika wa filamu hiyo

Mboto akiwa na mrembo
Mboto akiwa na mrembo

Mboto
Mboto

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW