Habari

Hukumu ya kesi ya Lulu kusomwa Novemba 13 mwaka huu (+Video)

Kesi inayomkabili muigizaji wa Filamu,  Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo alhamisi imeendelea kusikilizwa Mahakamani ambapo washauri watatu (Wazee) wa Mahakama Kuu wamesema mshitakiwa Lulu aliua bila ya kukusudia.

Washauri hao wametoa maoni yao leo Alhamisi Oktoba 26,2017 baada ya upande wa Jamhuri na wa utetezi kukamilisha kuwasilisha ushahidi.

Muigizaji, Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi ya kumuua aliyekuwa muigizaji wa filamu, Steven Kanumba bila kukusudia.

Lulu anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7,2012, nyumbani kwa Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam. Jaji Sam Rumanyika amesema hukumu itatolewa Novemba 13, mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents