Burudani ya Michezo Live

Lulu arudi chuo, anachukua Human Resources

Msanii mahiri wa filamu Elizabeth Micheal ‘Lulu’ amerudi chuoni na kuamua kuchukua kozi ya Human Resources.
Lulu

Muigizaji huyo ameweka wazi anachosomea baada ya mashabiki katika mtandao wa Periscope, kutaka kujua anasomea nini baada ya kupost video mbalimbali katika mtandao huyo huku akizungumzia maswala ya chuo.

“Jamani nimechoka kuulizwa nasomea nini, nasomea nini, nachukua Human Resources,” alisema Lulu.

Muigizaji huyo hakupenda kuweka wazi ni chuo gani anasoma, lakini aliweka wazi wiki hii naingia katika mitihani.

Lulu ni miongoni mwa wasanii wachache wa filamu walioamua kurudi darasani na kuongeza maarifa.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW