Burudani

Lulu: Ifike muda tutumie mitandao ya kijamii kusaidiana mawazo na sio kutukanana

Moja ya mambo sita tuliyoandika kuwa ni sababu ya watanzania kuupenda mtandao wa Instagram, ni kushuhudia matusi ambayo mastaa wanayavuna kutoka kwa followers wao.

10914374_855050391212726_1290368029_n

Lakini unadhani Instagram inapaswa kuwa sehemu ya kihuni kiasi hicho? Hapana.

Muigizaji wa filamu, Elizabeth ‘Lulu’ Michael anaamini hawezi kufikia malengo yake kwa mawazo yake pekee bali anahitaji msaada kutoka kwa vijana wenzake ambao nao wana nia na malengo kama yake katika kufikia ndoto zao. Ndio maana anahisi Instagram inaweza kuwa ni sehemu nzuri ya vijana kupenda michongo na sio matusi.

“Nikiwa Kama Kijana Mpenda Maendeleo, mwenye ndoto na malengo ya kufika mbali najua mawazo yangu peke yangu yanaweza yasitoshe mimi kufika ninapopataka,” ameandika kwenye Instagram.

“Najua wapo vijana wengi wenye nia kama yangu..!Nadhani umefika wakati wa kutumia mitandao ya kijamii Kwa kujengana na kusaidiana hasa ki mawazo Ili wote tuweze Kuwa sehemu fulani siku moja.”

Lulu ameonesha wazi kuwa hapendezwi na tabia ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii vibaya hasa kwa kudhalilishana.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents