Burudani

‘Lyricist Lounge’ kuadhimisha mwaka mmoja Jumamosi hii House Masaki

Tamasha ambalo hualika wasanii mbalimbali wakiwemo washairi, waimbaji na rappers, ‘Lyricist Lounge’, limetimiza mwaka mmoja tangu lianze.

Lyricist

Tamasha hilo huwaalika wasanii mbalimbali kutumia nguzo hizo za sanaa kuonyesha uwezo wao na kuwasiliana na watazamaji. Sherehe hizo za kutimiza mwaka mmoja zitafanyika House Masaki Jumamosi hii kuanzia saa moja jioni.

Directions

Grace Matata ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza huku washereheshaji wakiwa ni pamoja na Joe Legendary na Evans Bukuku.

Hakuna kiingilio.

Toka tamasha hilo lianzishwe, wasanii mbalimbali wametumbuiza wakiwemo Wakazi, Kiche, Sima, Langa, Mic Lon, Carol Kinashe, Lufu, Chi na wengine.

“Wale wapenzi wa Hip Hop waliowahi kufika kwenye event hiyo wakiwemo watu kama Master Jay, Shah, Mzungu Kichaa, Evans Bukuku wengi wao wamekuwa audience ya kudumu kwenye event hiyo wakijakuenjoy kuwasikiliza wasanii hao wengi wao wakiwa underground wakipata nafasi ya kutumia sanaa ya ushairi na muziki kuburudisha na kufikisha ujumbe wanaoutaka kwa audience,” yamesema maelezo kutoka kwa mmoja wa wahusika, Ben Kyambile.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents