Burudani

M-Rap ataja sababu ya kutoka B’Hits ni kuisha kwa mkataba wake na ugomvi wake na producer Pancho

Baada ya Vanessa Mdee, Gosby na Mabeste, M-Rap amekuwa msanii mwingine kutoka kwenye label ya B’Hits Music Group.

page

Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio leo, rapper huyo ambaye wiki hii ameachia ngoma yake mpya ‘Usiende Mbali’ aliyomshirikisha Jux, amesema kuisha kwa mkataba na ugomvi wake na producer wa B’Hits, Pancho Latino ndio sababu zilizomuondoa.

“Tayari nilikuwa nimeshamaliza mkataba wangu halafu kingine ni kwamba kulikuwa na misunderstanding na vitu vidogo vilitokea kati yangu na producer Pancho, vilitokea ni vitu vya kibinadamu kawaida lakini mimi tayari mimi nilishasamehe,” alisema.

Hata hivyo kauli ilitiwa chumvu na na DJ Kim aliyesema alisikia kuwa Pancho alimpiga M-Rap akiwa studio.

“Ni kweli ilitokea hivyo lakini mimi nilishasamehe kwahiyo yaani naendelea na mambo yangu tu,” alisema M-Rap.

Usikilize wimbo wake mpya hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents