Habari

Maadhimisho ya siku ya mtindio wa ubongo kufanyika Kitaifa Dar

Chama cha Wazazi na Watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo,Akili na Viungo Tanzania (CHAWAUMAVITA) kitafanya maadhimisho ya siku ya mtindio wa ubongo duniani kwa lengo la kuipa jamii uelewa juu ya changamoto wanazozipata watoto wenye matatizo hayo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama hicho, Hilali Said alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo ambapoa amesema lengo ni kuwaleta pamoja familia zinzolea watoto hao ili wabadilishane uzoefu.

Said amesema “Kwa kawaida Siku ya Mtindio wa Ubongo duniani huadhimishwa kila Jumatano ya kwanza ya mwezi Oktoba lakini kwa mwaka huu itaadhimishwa tarehe 6, ambapo yanategemewa kufanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mjimwema vilivyopo wilaya ya Kigamboni na tunategemea mgeni rasmi wa maadhimisho hayo atakuwa Mkuu wa Wilaya hiyo.”

“Nchi mbalimbali duniani huadhimisha siku hiyo kwa kutoa elimu ya ulemavu wa aina hiyo kwa wananchi ili kupunguza athari zinazojitokeza kwa wazazi na watoto wenyewe pamoja na kuwasaidia wanachama kutetea na kupata haki zao kwa mujibu wa sheria.”

Kwa upande wake mweka hazina wa chama hicho, Jane Kim ameiomba Serikali kuwasaidia watoto hao kwa kuwapatia mazingira mazuri ya kusomea pamoja na walimu wa kutosha wenye elimu stahiki ikiwa ni pamoja na kuwapatia ulinzi wa kutosha wanapokuwa shuleni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents