HabariUncategorized

Maafisa elimu 12 Dar watumbuliwa kisa posho

Mkuu wa Mkoa wa Dar esa Salaam, Paul Makonda Jumatano hii amekutana na wadau mbalimbali wa elimu ndani ya mkoa wa Dar es salaam na kujadili kwa pamoja sababu za kufeli kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ndani mkoa huo.

Afisa Elimu Mkoa, Hamisi Lissu aliwatumbua maafisa elimu 12 ambao walishindwa kueleza matumizi tsh 250,000 ambazo hupewa kila mwezi kama posho ya kazi.

Chanzo cha kuwasimamisha nafasi zao ni kutokana na kudai malipo ya posho zaidi ya ile wanayopewa hivi sasa ya kima cha shilingi laki mbili na nusu, fedha kwaajili ya posho ikiwa ni nje ya mishahara yao lakini wamelalamikia mbele ya mkuu wa mkoa kuwa haziwatoshi katika kufanya shuhuli zao za kimaendeleo ya elimu kwa kata zao .

Jambo ambalo lilipelekea kutofautiana baina ya maafisa elimu kata hao ambao jumla ya idadi yao ni 28 lakini hao 12 kati yao walikataa wakitaka kuongezewa kwa posho hiyo.

Hata hivyo Rc Makonda alimwagiza afisa elimu wa mkoa kuwavua vyeo vyao wote 12 na kuwapangia majukumu mengine kisha afanye utaratibu wa kujaza nafasi zao kwa haraka.

“Afisa nakuagiza hawa 12 wote washushwe vyeo vyao pamoja na kuwatafutia adhabu nyingine zaidi,serikali hii ya awamu ya tano haina fedha za kuwapa posho za kiti cha madaraka tofauti na wanazo pewa kwa sasa,tafadhali nenda kawapange wakawe waalimu wa kawaida kwenye shule ambazo zina uhaba wa waalimu,”Alisema Makonda

Awali ya yote wakuu wa shule za msingi na sekondari walipata hursa za kueleza changamoto zao na baadaye Mkuu wa Mkoa huyo kuzitolea ufumbuzi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents