Habari

Maafisa wa bandari Lebanon kifungoni kwa uzembe, zaidi ya watu 135 wapoteza maisha huku 300,000 hawana makazi baada ya mlipuko

Baadhi ya maafisa wa mji wa Beirut wamewekwa katika kifungo cha nyumbani huku wakisubiri uchunguzi kuhusu mlipuko mkubwa wa siku ya Jumanne, kulingana na serikali ya Lebanon.

Mlipuko huo uliwaua watu 135 na kuwajeruhi wengine 4000. Hali ya tahadhari ya wiki mbili imeanza kutekelezwa nchini humo.

Rais Michel Aoun alisema kwamba mlipuko huo ulisababishwa na tani 2750 za Amonium Nitrate iliokuwa imehifadhiwa katika ghala moja katika bandari ya mji huo.

Afisa mkuu wa masuala ya forodha Badri Daher alisema kwamba shirika lake lilitoa wito kwa kemikali hiyo kuondolewa, lakini hilo halikufanyika.

”Tumewaachia wataalamu kufichua sababu zake”, alisema. Amonium Nitrate hutumika kama mbolea katika kilimo na pia kama kilipuzi.

Katika kikao cha dharura cha baraza la mawaziri siku ya Jumatano, rais Aoun alisema: Hakuna maneno yanaweza kuelezea tishio ambalo limekumba Beirut usiku uliopita, na kuufanya mji huu kama uliokumbwa na janga.

Wataalamu katika chuo kikuu cha Sheffield nchini Uingereza wanakadiria kwamba mlipuko huo ulikuwa na kiwango cha 1/10 cha nguvu za bomu la nyuklia lililoangushwa katika mji wa Japan wa Hiroshima wakati wa vita vya pili vya dunia na limetajwa kuwa mlipuko mkubwa wa bomu lisilo la nyuklia katika historia .

rescuers in the port area, 5 Aug

Ni nini kilichosababisha mlipuko huo?

Ammonium nitrate imeripotiwa kuwa katika ghala hilo mjini Beirut kwa muda wa miaka sita baada ya kupakuliwa kutoka kwa meli iliokamatwa 2013.

Mkuu wa bandari ya Beirut pamoja na mkuu wa mamlaka ya forodha wote waliambia vyombo vya habari nchini humo kwamba wameandikia mahakama mara kadhaa wakiiomba kwamba kemikali hiyo iuzwe ili kuhakikisha usalama wa bandari.

Mkurugenzi mkuu wa Bandari Hassan Koraytem aliambia runinga ya OTV kwamba walikuwa wanafahamu kwamba bidhaa hiyo ilikuwa hatari wakati mahakama ilipoagiza ihifadhiwe katika ghala hilo, lakini sio kwa kiwango hicho.

blast aftermath, 5 Aug
 

Baraza kuu la ulinzi nchini humo limeapa kwamba wale watakaopatikana na hatia wataadhibiwa vikali.

Waziri wa uchumi Raoul Nehme aliambia BBC: “Nadhani ni kutowajibika na usimamizi mbaya na kuna wajibu mkuu kutoka kwa usimamizi na hata serikali zilizopita. Hatufikiria kunyamaza baada ya mlipuko kama huu kuhusu ni nani muhusika”.

 

”Kifungo cha nyumbani kitawashirikisha maafisa wote wa bandari , ambao walihusika katika suala la kuhifadhi Amonium Nitrate, wakiilinda na kusimamia usimamizi wake tangu Juni 2014”, alisema waziri wa habari Manal Abdel Samad.

Mzigo huo wa amonium nitrate uliwasili kupitia meli iliokuwa na bendera ya Moldova , kwa jina Rhosus ,ambayo iliingia katika bandari ya Beirut baada ya kupata tatizo la kiufundi wakati wa safari yake kutoka kuelekea Mozambique, kulingana na tovuti ya Shiparrested.com, ambayo inasimamia masuala ya meli.

Meli ya Rhosus ilikaguliwa na kupigwa marufuku kutoondoka baadaye kuwachwa na wamiliki wake, na hivyobasi kuzua tatizo la kisheria. Mzigo wake ulihifadhiwa katika ghala moja la bandari kwasababu za kiusalama.

https://www.youtube.com/watch?v=4nSEErp59zM

https://www.youtube.com/watch?v=1UmofRmlD50

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents