Michezo

Maamuzi ya Frank Lampard kumrejesha mkongwe Petr Cech kwenye kikosi cha Chelsea yako sahihi ?

Klabu ya Chelsea imethitisha kuwa Petr Cech katika amejumuishwa kwenye kikosi cha klabu hiyocha wachezaji 25 ambacho kitashiriki ligi kuu ya Uingereza msimu huu wa 2020/21.

Mlinda mlango wa Chelsea, Petr Cech kabla ya kutundika daruga.

Cech mwenye umri wa miaka 38 amejumuishwa kwenye kikosi hicho kama mchezaji huru na anaingia kikosini kama mchezaji wa dharula.

Mlinda mlango huyo alistaafu kucheza soka mwaka 2019, kwasasa ni mshauri wa ufundi na utendaji wa klabu ya Chelsea.

Kujumuishwa kwa Cech imeelezwa kama hatua ya tahadhari kutokana na hali ambazo hazijawahi kutokea kwasasa zinazosababishwa na mzozo wa Covid-19.

Alicheza zaidi ya michezo 300 tangu msimu wa 2004 hadi 2015 akishinda mataji makubwa 13 yakiwemo ya ligi kuu manne, FA manne na la ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2012 kabla ya kujiunga Arsenal.

Walinda mlango wengine waliopo kikosini ni pamoja na Eduardo Mendy, kepa Arrizabalaga na Willy Caballero.

KIKOSI HICHO LA LAMPARD HIKI HAPA:

Kepa Arrizabalaga
Antonio Rudiger
Marcos Alonso
Andreas Christensen – homegrown
Jorginho
Thiago Silva
N’Golo Kante
Tammy Abraham – homegrown
Christian Pulisic
Timo Werner
Willy Caballero
Fikayo Tomori – homegrown
Kurt Zouma
Edouard Mendy
Mateo Kovacic
Olivier Giroud
Mason Mount – under-21
Callum Hudson-Odoi – under-21
Ben Chilwell – homegrown
Hakim Ziyech
Billy Gilmour – under-21
Reece James – under-21
Cesar Azpilicueta
Kai Havertz – under-21
Emerson Palmieri
Petr Cech

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents