Burudani

Maana ya jina la mtoto wa kwanza wa Kanye West na mpenzi wake Kim Kardashian ‘North West’ yafahamika

Watu wengi wametoa maoni yao kuhusiana na jina alilopewa mtoto wa kike wa lovebirds Kanye West na TV star Kim Kardashian ‘North West’ na wengi wao wameonesha kutolifurahia sana jina hilo na kila mmoja amekuwa na sababu ya mtazamo wake, lakini sababu ya wapenzi hao kumwita mtoto wao jina hilo imefahamika.

Kim-Kardashian-and-Kanye-West

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na couple hiyo, wazazi hao wapya (Kanye na Kim) wameiambia familia yao kuwa jina North West kwao lina maanisha “highest power” (uwezo wa juu kabisa). “North is the most high. There is nothing higher than North. And, when it comes to the stars, the sun rises in the East and sets in the West,” chanzo hicho kiliuambia mtandao wa E! News.

Chanzo hicho kiliendelea kusema “look at her as being their highest point together. Nothing is more special than North. Kim keeps saying, ‘She is our North Star,’ ”

Ujio wa Baby North duniani umeongeza kitu kikubwa katika mapenzi ya Kanye West na Kim Kardashian ambao mwezi (September) wanategemea kufunga ndoa jijini Paris baada ya Kanye kutangaza ndoa kwa Kim hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents