Maandalizi ya tuzo za Kilimanjaro Music Award ndiyo yanafikia ukingoni ilikupisha tamasha zima la liweze kufanyika siku ya juma mosi Mach26 kwa mwaka huu 2011. Nafasi za kupiga kura zilishatolewa sehemu mbalimbali, ili kila mmoja apate nafasi ya kumpigia msanii anayempenda, ilikufanikisha kuwania tuzo katika kinyanyiro husika.
Hakika huwa ni siku ya furaha kwa msanii, ambaye amechaguliwa kuwa mshindi katika moja ya tuzo alizokuwa akiwania, na ndipo anapojua amekubalika kinamna gani kwa watu wake ambao wamefanikisha kwa yeye kupata tuzo hiyo.
Msanii anayepata tuzo hujijengea histori ya mwaka huo, ingawa wapo wasanii kila mwaka wanachukua tuzo na kutokuwa jambo la ajabu kupata tuzo, lakini bado inamletea furaha kwa tuzo hiyo.
Tofauti na miaka ya nyuma kama tulivyozoea, mwaka huu wameamua kujali wasanii wa ndani ambao watatumika katika kutoa buludani siku hiyo, tamasha badala ya wasanii toka nje. Ni jambo ambalo wasanii wamelipenda na wadau mbalimbali wameonekana kuliunga mkono, kwakuwa wao ndiyo wahusika wa tuzo basi hata katika kutoa buludani itabidi wahusike kuliko kutoa wasanii nje na kisha kutofikia ile buludani watu walioitarajia kutoka .
Vifaa vya bendi vikiwa tayari kwaajiri ya kutoa buludani kutoka kwa msanii husika
dj Akirekebisha vifaa, ilivisije vikawachachafya watu siku ya tamasha.
Mpangilio wa viti upo namna hii, karibu..
Hapa wakisogeza vifaa kwaajiri ya kutengenezea ngazi ya steji
Zamu ya taa kupanda juu,
Hata wakirekebisha chombo maalum kwaajiri ya Sinema ya ‘Live’
Wasanii wakiwa nje baada ya kupata somo kidogo la kuijua na kuisoma steji,
Kama kawaida hata msibani wapambe hawakosi, nasi tulikuwepo hapo kukuletea taarifa hii, ila kwa zaidi picha za na video za matukio yote tuungane kesho kwaajiri ya Tamasha lenyewe.