Burudani

Maandalizi ya ndoa ya Lulu na Majay yafikia patamu (Video)

Malkia wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ siku ya jana anadaiwa ametolewa mahari na mpenzi wake wa muda mrefu Majay ikiwa ni maandalizi ya ndoa yao mwisho wa mwaka huu.

Mrembo huyo amefanya sherehe hiyo ikiwa ni siku chache toka amalize hadhabu yake ya kifungo cha miaka 2 jela baada ya kukutwa na hatia na mahakama ya kumuua Steven Kanumba bila kukusudia.

Katika video ambazo zinasambaa mtandaoni zinamuonyesha mrembo huyo akimtambulisha mume wake huyo mjarajiwa kwa wazazi wake.

Taarifa zinazosambaa nitandaoni zinaeleza kwamba siku ya jana mrembo huyo alitolewa mahari na Majizo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ambaye ndiye msimamizi wa ndoa hiyo ametoa taarifa husiana na wawili hao kukutana siku ya jana.

“Mrembo Elizabeth Michael ‘Lulu’ siku ya jana anadaiwa ametolewa mahari na mpenzi wake wa muda mrefu Majizo ikiwa ni maandalizi ya ndoa yao mwisho wa mwaka huu,” alisema Makonda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents