Habari

Maandamano dhidi ya ujio wa George W. Bush

Mamia ya waislamu nchini Tanzania wameonekana wakiandamana kupinga ujio wa Raisi wa Marekani, Mheshimiwa George W. Bush ambaye anatarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ziara ya siku nne. [Bofya hapa kuangalia video ya maandamano hayo]

Maandamano

 

 

 

Mamia ya waislamu nchini Tanzania wameonekana wakiandamana kupinga ujio wa Raisi wa Marekani, Mheshimiwa George W. Bush ambaye anatarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ziara ya siku nne.

 

Tukio hilo lililofanyika leo mara tu baada ya waumini hao kumaliza kuswali swala ya Ijumaa, kundi hili la waislamu wanaoonekana kuwa na msimamo mkali, walionekana wakikatiza katika Bara bara ya Ali Hassan Mwinyi wakielekea ulipo ubalozi wa marekani huku wakinadi kwa sauti ya juu zaidi wakisema “Nani gaidi, ‘Bush’, Nani muuaji ‘Bush’ na mengi zaidi yaliyokuwa yakiashiria kupinga kwa ujio wa raisi huyo huku shughuli ikiongozwa na Amiri wa shura ya maimamu nchini Sheikh Khamisi Kundecha wa msikiti wa Idrissa karakoo..

 

Aidha malengo ya ziara ya raisi huyo ni kuja kusaidia kupigana vita dhidi ya ugonjwa wa Malaria na Ukimwi, magonjwa ambayo yanaonekana kuinyanyasa sana jamii ya kitanzania naafrika kwa ujulma.

 

 

 

Bofya hapa kuangalia video ya maandamano hayo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents