Habari

Maandamano Hong Kong yafikia pabaya, Mmoja afariki dunia ‘Tutalipiza kwa kuchoma moto vituo vya Treni’

Waandamanaji jijini Hong Kong, Jana Jumapili wamevunja madirisha katika kituo cha treni cha chini ya ardhi na eneo la maduka kufuatia kifo cha mwandamanaji mwenzao aliyeuawa Ijumaa ya wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Shirika la Associated Press, Limeripoti kuwa watu kadhaa walikamatwa na polisi kwa kujihusisha na vurugu hizo.

Mishumaa iliwashwa na usiku wa maombi ulifanyika sehemu mbalimbali za jiji hilo, Katika kuomboleza kifo cha muandamanaji mwenzao ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Hong Kong, Chow Tsz-Lok, 22, aliyekuwa anasomea masuala ya sayansi na teknolojia.

Waandamanaji hao ambao walikuwa na ghadhabu, Walishika mabango yaliyosmeka ‘Tutalipiza kifo cha Chow, Kwa kuchoma moto vituo vya Treni’.

Polisi walijaribu kuwaondosha waandamanaji kutoka katika eneo hilo na walitupa mabomu ya machozi kadhaa ili kuwatawanya.

Imeripotiwa kuwa Chow ndiye mtu wa kwanza kufariki dunia katika kipindi cha miezi mitano ya maandamano hayo, Ambapo waandamanaji wanadai kuwepo serikali ya kidemokrasia na mabadiliko katika sera.

Rais wa chuo kikuu cha Hong Kong, Wei Shyy ametaka uchunguzi huru na wa kina ufanyike kujua ni katika mazingira gani Chow alifariki.

Picha za video zinazotumwa kwenye mitandao ya kijamii, Zinaonyesha polisi wakizuia gari la wagonjwa kuingia eneo hilo.

Polisi wamekanusha tuhuma dhidi yao kwamba walizuia gari la wagonjwa au walimkimbiza Chow, na kusababisha apate majeraha. Polisi wanataka suala hilo lisikilizwe na jopo la wachunguzi wa serikali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents