Habari

Maandamano: Watu 9 wakamatwa Dar, diwani wa CHADEMA akamatwa Iringa

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu tisa waliokuwa wakiandamana eneo la Samora Avenue Posta, Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa watu hao. Kukamatwa kwao kumekuja mara baada ya Jeshi la Polisi kuonya kuwa litawachukulia hatua kali wale wote watakaokaidi agizo la kutoandamana kama walivyoagiza.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia kwa mahojiano Diwani wa Kata ya Igumbiro, Musa Mlawa kwa kosa la kufanya mkusanyiko usio halali.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire Diwani huyo anashikiliwa kwa mahojiano ili kubaini chanzo cha mkusanyiko huo.

Soma Pia; Rais Magufuli atoa onyo kali kwa watu wanaopanga kuandamana

Utakumbuka Rais Magufuli, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba walishaonya kuhusu maandano hayo yaliyokuwa yapengwa kufanyika leo April 26, 2018. Kwa asilimia kubwa maandamano hayo yalikuwa hakihamasishwa kupitia mitandao ya kijamii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents