Habari

Maandamano ya Hong Kong kuwakutanisha Rais wa Marekani na Xi Jinping wa China, Trump aandika ujumbe huu

Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kufanya mkutano binafsi na rais wa China Xi Jinping kujadili mzozo wa kisiasa unaoligubika eneo la Hong Kong.

US President Donald Trump with Chinese President Xi Jinping

Katika ujumbe kwenye twitter, Trump amesema hana shaka hata kidogo kwamba Bwana Xi anaweza” kutatua kwa huruma mzozo wa Hong Kong.”

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Amehusisha pia maandamano hayo na mpango wa biashara wa Marekani na Beijing, wakati hali ya wasiwasi wa kibiashara ikiendelea.

“Bila shaka China inataka makubaliano. Basi washirikiane kwa ubinaadamu na Hong Kong kwanza!” aliandika kwenye twitter.

Matamshi ya Trump yanajiri baada ya maandamano ya wiki kadhaa ya kutetea demokrasia yaliozushwa na upinzani kupinga mswada wa kuhamishwa kwa wahalifu kushtakiwa nje ya Hong Kong.

Wakosoaji wanahofia mswada huo huenda ukaifanya Hongkong kuzidi kuwa chini ya udhibiti wa China.

Mswada huo umesitishwa kwa sasa, lakini maandamano yamegeuka na kuwa vuguvugu la kuunga kwa ukubwa demokrasia.

Hong Kong ni sehemu ya China chini ya mfumo wa “Taifa moja, mifumo miwili” inayoipatia mamlaka ya juu ya kujitawala.

Ina mfumo wake wa sheria na mahakama na ina uhuru kadhaa usiokuwepo katika eneo kuu – Mfano Hong Kong na Macau fondio maeneo ya pekee katika ardhi ya China ambapo watu wanaruhusiwa kukusanyika kukumbuka maandamano ya bustani ya Tiananmen.

Wasiwasi na gesi ya kutoa machozi

Wasiwasi kati ya waandamanaji na maafisa wa polisi umeongezeka katika siku za hivi karibuni.

Jana Jumatano serikali ya China imeshutumu vikali waandamanaji , na kutaja tabia yao ‘kukaribia ugaidi’.

Ilipofika jioni, polisi waliojihami kwa nyenzo za kudhibiti fujo walifyetua gesi ya kutoa machozi dhidi ya mamia ya waandamanaji waliokusanyika katika mtaa wa Sham Shui Po waliokuwa wakingarisha taa nyekundu za laser dhidi ya kituo cha polisi kama njia ya kulalamika.

Taa hizo za laser zimepata umuhimu katika maandamano hayo baada ya mwanafunzi aliyekuwa akiandamana kukamatwa na polisi kwa kumiliki taa hiyo, ambayo maafisa walisema ni “silaha ya kutusi” ambayo inaweza kusababihsa majeraha mabaya ya macho.

Tangu hapo, waandamanji wametumia taa hizo kama njia ya kuwakejeli maafisa kwa tuhuma hiyo.Protesters using laser pointers during a demonstrationWaandamanaji wanatumia taa zenye mwanga mkali kama njia ya kuandamana

Ghasia hizo zimejiri siku moja baada ya maandamano katika uwanja wa kimataifa wa ndege Hong Kong kukumbwa na vurugu Jumanne usiku.

Maelfu ya waandamanaji walimiminika katika viingilio vya uwanja huo wa ndege na kutumia magari ya magurudumu ya kubeba mizigo kama vizuizi.

Yalianza kama maandamano ya amani lakini baadaye yakageuka na kukumbwa na ghasia baada ya maafisa wa polisi kuwapulizia pilipili baadhi ya waandamanaji walipojaribu kuingia katika lango kuu la uwanja huo wa ndege kusaidia kumuondoa mwanamume aliyejeruhiwa.

Ghasia zilizuka ghafla baina ya pande hizo mbili na katika tukio moja, afisa anayetuhumiwa kumshikilia kwa nguvu mwanamke alionekana kwenye kamera akiwapiga waandamanaji.

Alielekeza kiholela bunduki yake dhidi ya umati uliokuwepo kuwatawanya, kabla ya kuondoshwana maafisa wenzake .

Huku ghasia zikitatiza miundo mbinu Hong Kong na kukiwa hakuna suluhu ya hivi karibuni, wanaharakati wanaohfia jeshi la China litaingilia kati moja kwa moja mzozo huo – licha ya kwamba baadhi ya wachambuzi wanadhani hilo haliwezekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents