Habari

Mabadiliko ya katiba yamtaka Rais Rodrigo Duterte asigombee tena urais, mwenyewe asema watapata tabu sana

Ombi la pendekezo la mabadiliko ya vifungu vya katiba vya kumtaka Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte kugombea tena Urais kwa awamu ya pili limegonga mwamba na badala yake hataruhusiwa kugombea tena Urais muhula wa pili.

Image result for Duterte 2022
Rodrigo Duterte

Mabadiliko hayo yaliyotangazwa na Jaji Mkuu Mstaafu wa Taifa hilo, Reynato Puno Jumatatu ya Julai 16, 2018 yamemzuia Duterte kugombea Urais kwa muhula wa pili huku baadhi ya vifungu vikimpa ahuweni Rais huyo mwenye maneno makali kwa wakristo.

Hata hivyo, duru za habari nchi Ufilipino zinasema kuwa Rais Duterte hajastushwa na taarifa hizo na Chama chake kimesema kitafanya kila liwezekanalo kiongozi huyo kugombea tena urais mwaka 2022.

Taarifa hizo za Duterte kuonesha nia ya kutaka kuongoza tena kwa muhula wa pili kwa nguvu zimepuuzwa na Rais Mstaafu wa taifa hilo, Aquilino “Nene” Pimentel Jr. ambaye amesema kuwa anamfahamu na atamshauri Duterte asing’ang’anie Madaraka na aheshimu katiba.

Mwezi uliopita Duterte aliwakasilisha wakristo nchini humo baada ya kunukuliwa akimdhihaki Mwenyezi Mungu kuwa ni ‘MPUMBAVU’.

SOMA ZAIDI – Baada ya kumtukana Mungu, Rais Duterte akataa kuwaomba radhi Wakristo ‘Mungu wenu simjui namjua Allah’

Kwa mujibu wa gazeti la GMA la nchini Ufilipino limeeleza kuwa Duterte na Chama chake amepanga kujiuzulu urais miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2022 ili aweze kugombea tena kwani kikatiba inaruhusiwa.

Katiba ya Ufilipino hairuhusu Rais wa nchi hiyo kugombea urais mihula miwili mfululizo na Duterte analiongoza taifa hilo lenye  Wakristo wapatao milioni 88 hadi mwaka 2022.

SOMA ZAIDI – Rais wa Ufilipino amkashfu Mungu ‘mpumbavu, alitegemea nini kuwaumba Adam na Eva’

Chanzo: Gazeti la INQUIRER

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents