Moto Hauzimwi

Mabaga Fresh

Mabaga FreshBaada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, mabaga fresh wameamua kutoka kikamilifu ambapo wameweka wazi sababu zilizopelekea kundi hilo kukaa kimya kwa muda mrefu

 

Mabaga Fresh

 

 

Na Daniel Nyalusi

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, mabaga fresh wameamua kutoka kikamilifu ambapo wameweka wazi sababu zilizopelekea kundi hilo kukaa kimya kwa muda mrefu sana ni maandalizi ya ujio mpya ambao unatarajiwa kuwa na mabadiliko makubwa sana .

“Unajua kusikika sana saa nyingine hupelekea wapenzi kuwachoka kwani kama msanii unatakiwa kuwa na muda wa kutosha wa kufanya maandalizi, tunajua kuwa wapenzi wamekuwa na hamu sana ya kusikia kazi zetu mpya” alisema Juma Nne a.k.a JB a.k.a Mbuzi wa albadir a.k.a Mkuu wa Majaji.

Pamoja na hayo vijana hawa ujio wao wa hivi karibuni umetengeneza familia yao ambayo inatarajiwa kuwa ni tishio katika muziki, litakalokwenda kwa jina la ‘watega mabomu’ “lengo la kundi hili ni kuwasaidia wasanii wakali ambao bado hawajatoka ila tunaamini kwa ujio huu lazima watoke” Dj Snox.

Hivi sasa wanatarajia kuja na albam yao kama ‘mabaga Fresh’ na baadae wanatarajia kutoka kama ‘watega mabomu’ ambapo watakuja na staili yao mpya uchezaji itakayojulikana kama ‘FULL MIKAZO’

Albam yao itakuwa na jumla ya nyimbo nane na itakwenda kwa jina la ‘Jeuri ya Fedha’ na itakuwa ni albam yao nne “ukweli hivi sasa tumeamua kufanya muziki wa hip hop zaidi japo kuna kipindi tuligusia hata aina Fulani ya muziki kama Dancehall n.k ila kwa sasa tumeamua kutoka kama enzi za ‘mtulize’ au tunataabika.

Albam nzima itafanyiwa katika studio za mawingu chini ya muandaaji Boni luv, wameamua kurudi kufanya kwani huyu ndiye prodyuza pekee aliyewatoa kwa kuwaweka katika ramani ya muziki wa kizazi kipya kwa kuwafanyia jiwe lao ambalo halichuji la ‘mtulize’

Walizitajaa badhi ya ngoma zinazopatikana katika albam yao hiyo ni pamoja ‘Maisha ya kisela’ wakiwa na YP, ‘Naona Poa’ na Mh Temba na Jebi, ‘Mshkaji Kadata’ waliyofanya na Chege, ‘Mtu Shazi’ na mtu mzima Sir Nature na nyingine kibao.

{mos_sb_discuss:6}

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW