Michezo

Mabao matatu Ibrahim Ajib yampa kiburi hiki

Klabu ya Yanga inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikiwa na alama sawa na vinara Simba SC wakitofautiana kwa mabao katika msimamo huo.

Katika mchezo wa Jumamosi iliyopita klabu ya Yanga ilichomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, Bukoba huku mchezaji Ibrahim Ajib akionyesha mchango mkubwa katika kikosi cha Mzambia, George Lwandamina.

Ibrahim Ajib Migomba akichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo wakati alipoiwezesha Yanga kuchomoza na ushindi huo wa mabao 2-1 wakiwa huko Kaitaba dhidi ya wana tam tam klabu ya Kagera Sugar na kudhihirisha thamani yake na ubora aliyokuwa nao.

Katika mchezo huo wa wikiendi hii iliyopita kiungo huyo wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Ajib alivua jezi yake na kuianika ikiwa ni ishara ya kuonesha mashabiki jina na namba yake kitendo ambacho wachambuzi wa soka wanakilinganisha na walivyowahi kufanya wafalme wa soka duniani, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wakiwa katika ubora wao.

Swala ambalo lilozua maswali mengi kwa mashabiki na wadau wa soka kwa kutaka kulinganisha kiwango cha Ibrahim Ajib na wakali hawa kama anastahili kujifananisha nao.

Ibrahim Ajib Migomba mpaka sasa amefunga jumla ya mabao matatu kati ya sita ambayo timu yake ya Yanga imefunga huku akiwa anaongoza katika chati ya wafungaji wa klabu hiyo katika michezo yote iliyocheza msimu huu.

Bao lake la kwanza mara tu baada ya kusajiliwa na Yanga SC lilikuwa la ugenini dhidi ya Njombe Mji na kuweiwezesha timu yake kuchomoza na ushindi huo muhimu wa 1-0 katika safari ya kutetea Ubinwa wake wa ligi kuu.

Ajib akiiwezesha tena  Yanga kuchomoza na ushindi dhidi ya Ndanda FC kwa bao 1-0 lililodumu hadi dakika 90 ya mchezo na kuwa la pili toka kusajiliwa ndani ya  kikosi hiko cha wanajangwani.

Na bao lake la tatu ambalo limeifikisha Yanga SC  katika  nafasi hiyo ya pili ni dhidi ya Kagera Sugar huku akimsaidia Obrey Chirwa kufunga la utangulizi .

Ibrahim Ajib amesajiliwa na Young Africans kwa mkataba wa miaka miwili akitokea kwa mahasimu wao Simba SC  amekuwa na msaada mkubwa kwa vijana hao wa Jangwani kutokana na kipaji chake cha asili alichojaaliwa nacho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents