Mabasi ya Mwendo kasi 2010

Ule mradi wa wakala wa usafiri wa haraka nchini, DART unatarajiwa kutekelezwa kwa awamu sita ikiwa ni kabla ya kukamilika rasmi na hivyo kuwa wa kwanza na wa aina yake barani Afrika.

Ule mradi wa wakala wa usafiri wa haraka nchini, DART unatarajiwa kutekelezwa kwa awamu sita ikiwa ni kabla ya kukamilika rasmi na hivyo kuwa wa kwanza na wa aina yake barani Afrika.

Aidha, imeelezwa awamu hizo sita zitajumuisha barabara za Morogoro, Kawawa, Msimbazi na Sokoine, ambazo zote kwa pamoja zitakuwa na urefu wa kilometa 21, huku abiria zaidi ya 380,000 watakuwa wakisafirishwa Jijini kwa siku na mabasi makubwa 300 na madogo 147.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi huo, Bw. Cosmas Takule, wakati akizungumza na waandishi ofisini kwake Jijini.

Amesema usanifu wa mradi huo unahusisha njia maalum za mabasi zenye urefu wa kilometa 21 na vituo vikuu vya mabasi vitano ambavyo ni Kivukoni, Kariakoo, Ubungo, Moroko na Kimara.

Amesema vituo vingine vidogo vitakuwa 29 ambavyo ni vya kupandia na kushusha abiria huku pia kukiwa na vituo vikuuu viwili vya maegesho ya mabasi hayo ya haraka.

Akasema kuwa eneo la Kariakoo linatarajiwa kujengwa kituo kikuu cha mabasi hayo. Alidai ujenzi wa miundombinu ya mradi huo unatarajia kuanza Septemba 2008 na kuchukua takriban miezi 24 kumalizika, yaani Septemba mwaka 2010.

Aidha huduma ya usafiri chini ya mfumo huu mpya umepangwa uanze rasmi mwishoni mwa mwaka 2010.

 Akifafanua juu ya taratibu za malipo kwa watu ambao majengo na ardhi zao zitaathiriwa na mradi huo, Bw. Takule amesema kuwa wote watalipwa na kwa kuanzia, wale wa eneo la Gerezani Kota wataanza kulipwa mwezi huu, yote hii ikiwa ni kamilisha azma hii.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents