Burudani

Mabeste aanza kutoa semina kwa wasanii wachanga

Rapper Mabeste ameanzisha semina za kuelimisha wasanii wachanga pamoja na watu wa kawaida kupitia changamoto alizozipitia katika maisha ya muziki wake.

mabeste

Mabeste ameiambia Bongo5 kuwa tayari ameshaanza semina hizo katika mkoa wa Morogoro.

“Mimi hapa nilipofika nimeona nina mapungufu mengi ambayo yamesababisha nishindwe kufikia malengo yangu katika muda muafaka,” amesema.

“Nimeona nikikaa na mtu ambaye anataka kuanza safari nikawaeleza mfumo ukoje, unataka nini, itawasaidia sana kufikia malengo yao kwa sababu tayari wameshamfahamu adui wao. Ni bora kupambana na adui unayemjua kuliko usiyemjua. Kwahiyo nimejipanga kufanya hivyo sehemu mbalimbali za Tanzania yetu hasa kwenye vyuo. Nitakuwa nazunguka na kuwapa semina mbalimbali ambazo zitawasaidia.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents