Burudani

Mabeste adai haumii muziki kutomlipa

Rapper Mabeste amesema haumizwi kichwa na kutopata pesa kutokana na muziki wake anaoufanya sasa.

12080521_1157684377593107_1110025585_n

Mabeste ameiambia Bongo5 kuwa ameamua kuitengeneza kwanza brand yake mpaka afike kwenye standard nzuri.

“Kutopata pesa kwenye muziki hakunifanyi kuwa na stress kwa sababu my plan si kujitengeneza ili ninapotoa ngoma nipate hapo hapo, ila mimi nimejitengeneza kwa ajili ya baadaye,” amesema Mabeste.

“Nipo kwenye hii project ya muziki kwa sababu ya kumtengeneza Mabeste wa baadaye, afike kwenye nafasi ya juu lakini ni kwa kipindi fulani cha miaka. Kwahiyo nimejiwekea malengo makubwa na siangalii leo tu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents