Burudani

Mabeste awachana wasanii wenzake wanaodandia siasa

Mabeste ametoa ushauri kwa wasanii wenzake ambao wanajiingiza kwenye siasa na kusahau majukumu yao kwenye muziki.

Akizungumza na kipindi cha Mega Mix cha Abood FM, muimbaji huyo amesema, “Tufanye muziki,tusiconcetrate na siasa. Politics sasa hivi imeshika kuliko kitu kingine chochote na mpaka inasababisha baadhi ya artists kuachia track na zinakuwa zinafeli kwa sababu tu raia wamefocus sana kwenye politics kuliko burudani.”

“Unakuta sisi wasanii wengine tunaona ilituweze kutake attention na sisi lazima tufanye nyimbo za siasa ili raia waweze kuzisikiliza. Mimi naona tukae kwenye vipaji vyetu. Huo ni upepo tu, sio kila siku watu watatazama kitu kimoja tu,” ameongeza.

Muimbaji huyo ameahidi kuachia wimbo wake mpya ujulikanao kama ‘Wapungu’ ,ambao umetayarishwa kwenye studio za Kili Records.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents