Burudani

Mabeste: Je mbona B’Hits wametumia mistari yangu wakati mimi siko B’hits? Amtetea M-Rap

Baada ya mkataba wa kufanya kazi baina ya rapper M-Rap na studio iliyokuwa ikimsimamia kimuziki B’Hits Music Group kuingia dosari wiki iliyopita, msanii aliyewahi kuwa chini ya studio hiyo mpaka walipokuja kutofautiana na kusitisha kufanya kazi miezi kadhaa iliyopita, Mabeste ameonesha kusikitishwa na kilichomtokea M-Rap.

mabestee

Mabeste ambaye amekuwa kimya kwa muda sasa ametumia akaunti yake ya Facebook kuelezea baadhi ya mambo yaliyomsikitisha kuhusiana na sakata la B’Hits na M-Rap.

Hiki ndicho alichoandika:

Nasikitika Pancho Latino na Uongozi wa Bhits kwa kulalamika kua M-Rap ametumia mistari yao katika Track yake aliyoifanya Am Records (usiende mbali) kuwa ametumia Verse alizowahi kuandika kipindi yuko Bhits na kuamua kutoa hiyo Track yenye hiyo Verse ambayo ni (only you remix)… sasa mbona (only you remix) waliyoitoa Bhits ile chorus aliyoifanya Jux niliandika mimi wakat niko Bhits!! Je mbona wao wametumia mistari yangu wakati mimi siko Bhits? Na kama issue ni Copy n Paste au kuishiwa na idea,mbona beat iliyotumika kwenye Track yangu ya “SIRUDI TENA” Pancho amei Copy kwenye Track ya (cheap monkey ft chriss brown – champion)?? Je ni haki wanachofanya??
Ama wanataka kumuaibisha tuu dogo(M-rap), mbona wao pia wanazingua nao???
#MabesteArmy!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents