Burudani

Mabeste: Nafikiria nitengeneze home studio niwe nafanya kazi zangu nyumbani (Audio)

Baada ya kuwa miongoni mwa wasanii watatu walioachana na management ya B’Hits Music Group hivi karibuni , msanii aliyehit na single ya ‘Baadae Sana’ Mabeste amezungumzia mipango ya kazi yake ya muziki baada ya kutoka B’Hits.

IMG_6609

Akizungumza na Radio Free Africa ya Mwanza kupitia kipindi cha Show Time New Chapter, Mabeste amesema kuachana kwake na B’Hits kumeleta changamoto kubwa kwake hasa katika swala la uhuru aliokuwa nao katika kufanya kazi.

“Siwezi kusema kutoka ndani ya B’Hits sijapata kasoro, nimepata kasoro mapungufu ambayo nimeyapata ni mengi tu, kwamba sasahivi inabidi nitafute studio ambayo ninaweza nikakaa nikawa huru”, alisema Mabeste.

Moja ya mipango aliyonayo hivi sasa ni kuja kutengeneza studio yake ya nyumbani ili imrahisishie kuwa anafanya kazi zake kwa uhuru kama alivyoishazoea

“Kama sasahivi nina plan mi mwenyewe hapa nyumbani kwangu ninapo kaa kuna stoo nyuma nilikuwa ninafikiria nimuite fundi aje atoe hizo vitu, nijaribu kuahamishia kwenye nyuma ya nyumba yangu niweke studio, ni as in kwasababu mimi nilikuwa nimeshazoea mazingira ya kufanya kazi peke yangu, kufanya kazi niko studio nimechill sina usumbufu na mtu nakaa studio 24hrs ndio mazoea yangu tangia zamani.” Alisema

“Kwahiyo hata nafikiria nitengeneze home studio niwe nafanya kazi zangu nyumbani, nikienda natafuta studio ya mtu nikienda nakuwa nishaaenda na package yangu nzima sana sana naenda kuingiza vocals tu.”

Hata hivyo Mabeste amesema hiyo ni mipango ya ‘baadae sana’ ambayo inahitaji muda wa kujipanga hivyo haiwezi kuwa hivi karibuni,

“Lakini pia hizo ni plan ambazo bado nazifikiria bado sikajaa nika settle….nahitaji kurelax kufikiria nitaanza vipi kwasababu mwisho wa siku nikitoka bila kufikiria nita bugi.” Alimaliza Mabeste

Msikilize hapa

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/122115555″ width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents