Mabifu yaendelee, Kwani yanachangamsha muziki wetu ila tusiuane – Ommy Dimpoz

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amesema kuwa tofauti za wasanii wa Bongo Fleva au Bifu ziendelee kwenye tasnia hiyo kwani kwa namna moja zinakuza na kuchangamsha muziki wetu.

Akiongea na Bongo5, Ommy amesema kuwa biashara ya muziki sio kama biashara ya nyanya hivyo hata ushindani wake ni mkubwa kwa hiyo vitu kama bifu vinaweza vikatumika kuuza kazi zako zaidi.

Biashara ya muziki haiwezi kuwa kama biashara ya nyanya, Lazima kidogo kuwepo na bifu ile ya kuchangamsha gemu. Ndio maana unaona kuna vitu kama ‘Penseli’ kwa hiyo ni vitu vizuri ila tusiuane tu,“amesema Ommy Dimpoz.

Mwaka jana, Ommy Dimpoz aliingia kwenye vita ya maneno na msanii mwenzake Diamond Platnumz jambo ambalo mpaka leo limewafanya wawili hao kuishi maisha ya Chui na Paka.

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW