Habari

Mabucha 50,000 yafungwa Dar

Zaidi ya maduka 50,000 ya kuuza nyama jijini Dar es Salaam, yamefungwa kufuatia walaji wa kitoweo hicho kususa kula kutokana na ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa (RVF), imebainika.

Na Godfrey Monyo

 
Zaidi ya maduka 50,000 ya kuuza nyama jijini Dar es Salaam, yamefungwa kufuatia walaji wa kitoweo hicho kususa kula kutokana na ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa (RVF), imebainika.

 

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwenye maduka mbalimbali ya kuuzia kitoweo katika maeneo ya Mwananyamala, Buguruni, Manzese,Temeke na Mbagala, umebaini kuwa, idadi kubwa ya maduka hayo yamefungwa.

 

Kufungwa kwa maduka hayo kumechangiwa na bidhaa hiyo kuporomoka kwa soko lake kutokana na kuwepo kwa ugonjwa huo ambao hadi sasa umeua watu 89.

 

Mwenyekiti wa Umoja wa Wauza Nyama mkoani Dar es Salaam (UWANDA), Bw. Maulid Kivea alikiri kufungwa kwa mabucha hayo.

 

Aliongeza kuwa, jiji la Dar es Salaam lina zaidi ya maduka ya nyama 75,000 ambayo awali yalikuwa yakiuza bidhaa hiyo.

 

Alifafanua, kuwa, hali hiyo hivi sasa imebadilika kwa kiasi kikubwa na kusababisha kubaki maduka 20,000 tu.

 

�Hali inatisha, hata nikikwambia mimi nina maduka 12, lakini yote nimeyafunga kutokana na ukweli kwamba nyama hainunuliwi, � alisema Bw. Kivea.

 

�Tunachofanya ni kwamba, tunanunua ng`ombe kutoka mikoani na tunapowafikisha hapa, tunawaweka kwenye mazizi na gharama ya kumtunza ng�ombe ni kubwa lakini akichinjwa, watu hawanunui hivyo hakuna namna ni bora kufunga,� alisema.

 

Mwenyekiti huyo alisema kufungwa kwa maduka hayo kumesababisha wafanyabiashara wengi kubaki bila kazi huku wakikabiliwa na madeni.

 

Alisema awali walikuwa wakichinja ng�ombe 800 hadi 900 jijini Dar es Salaam, lakini kwa sasa kiwango hicho kimepungua mno.

 

Naye muuza nyama wa reja reja, Bw. Hassan Mlamba alisema ameamua kufunga kwanza duka lake hadi hapo tishio la RVF litakapotoweka.

 

Aliongeza kuwa, anahofu mtaji wake kwa kuwa utamalizika kwa kuwa kabla ya tishio la ugonjwa huo, alikuwa akiuza wastani wa kilo 100 kwa siku lakini sasa anauza chini ya kilo 30.

 

Bw. Mlamba alisema ndugu zake wengine wamelazimika kurudi nyumbani kwao Dodoma kutokana na ukweli kuwa wakiendelea kukaa hapa bila kazi, maisha yatazidi kuwa magumu.

 

Aliongeza kuwa, endapo hali hiyo itaendelea kuwa hivyo, watakuwa katika hali ngumu zaidi na pengine kushindwa kulipia kodi ya pango.

 

Kwa upande wa wateja wa nyama walisema tishio la RVF limechangia kwa kiasi kikubwa kuachana na ulaji wa kitoweo hicho.

 

Mmoja wa wateja hao, Bw. Walter Makwela, mkazi wa Mbagala alisema tangu kutangazwa mlipuko wa ugonjwa huo, hajawahi kula nyama pamoja na familia yake.

 

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents