Mabwawa saba azama mtu

mabwawa_1
KATIKA mabwawa ambayo yapo maeneo ya Mabibo mwisho yanayojulikana maarufu kama Mabwawa Saba,  leo asubuhi inasemekana katumbukia mtu ambaye inadaiwa ni mwanamke. Shuhuda mmoja ambaye alikuwepo hapo tangu asubuhi, amedai kwamba hadi kufikia saa kumi na nusu bado hajapatikana.

 

Aidha alidai kwamba  zilikuja gari la Uokoaji (Fire), na Amburace lakini hayakuweza kufanya chochote kutokana na mabwawa hayo kujaa tope, na kushindikana kabisa kufanikisha suala la kuokoa mwili huo.

mabwawa

Hata hivyo  Shuhuda huyo amesema mabwawa hayo ambayo yamekuwa yakipokea maji kutoka sehemu ya kiwanda , ambacho wengi hawajui ni kiwanda gani. Alidai kwamba Mabwawa hayo  yamekuwa ni kawaida kwa kila  mwaka kuua kutokana na watu kutumbukia kutokana na ulevi, ama hasira zilinazopelekea kujitumbukiza.
mabwawa_2

Anasema hii inatokana na mabwawa hayo kuwa karibu kabisa na makazi ya watu, ambapo watoto, mifugo na watu wazi,ma kupita maeneo hayo kwa kuelekea sehemu mbalimbali.
mabwawa_3

Hadi naondoka maeneo hayo, watu bado wanasubiri kuibuka kwa mwili wa mtu huyo baada ya kushindwa kuuopoa kutokana na hari ya mabwawa hayo, kujaa tope.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents