DStv Inogilee!

Machangudoa wa Zimbabwe wakusanya mbegu za kiume na kuziuza kwa gharama kubwa

Wanaume wasio waaminifu walionywa mwaka jana nchini Zimbabwe kutoka miji ya Gwanda na Beitbridge iliyopo mpakani mwa Zimbabwe na Afrika ya Kusini.

Prostitute+sex+worker

Machangudoa kutoka miji hiyo hukusanya mbegu za kiume na kwenda kuziuza nchini Afrika ya Kusini. Inasadikika kuwa mbegu hizo zinakwenda kwa waganga wa kienyeji maarufu kama sangoma ili kutumika kwa mambo ya kishirikina.

Wengine wakihisi kwamba wanawake hao huuza mbegu hizo kati ya dola 25 hadi 30 kwa chupa ya milimeta 250 yaani robo lita. Wengine wanatafuta bei ya juu zaidi huko Dubai.

Machangudoa hao wanaofanya biashara hiyo walikumbana na wakati mgumu Oktoba 2014 baada ya mwanamke mmoja kutoka mji wa Gweru alipokamatwa na polisi akiwa na kondomu 31 zilizojaa mbegu za kiume zikiwa kwenye mfuko wa plastiki.

Mwanamke huyo baada ya kupelekwa mahakani alisema ya kuwa kondomu hizo huzipata kutoka kwa machangudoa wanaowajua ambao na wao huzikusanya kutoka kwa wateja wao.

Kutokana na hali hiyo kuna kesi nyingi za wanaume walioweza kubakwa na wanawake kwa imani za kishirikina kati ya miji kama Midlands, Harare na Mkoa wa Masvingo.

Mwanamme mmoja aliyeonekana kufedheheshwa na kitendo hicho alisema, “wanaume wengi wamechanganyikiwa baada ya kusikia habari hiyo hasa wale viruka njia kuona kwamba wamefanya ni biashara. Matumizi ya mbegu hizo hayajajulikana ingawa inasemekana yanatumika kwa ajili ya mambo ya kishirikina na Sangoma huko Afrika ya Kusini.

“Kuna wakati wiki iliyopita kuna jamaa mmoja alikuwa hajiwezi na kuwa kama amepoteza fahamu baada ya kumchukua changudoa na kwenda naye nyumba ya wageni. Wengi wanasema inawezekana alipewa madawa ili afanye tendo hilo mara nyingi zaidi ili kuvuna mbegu hizo.”

Wengi walisema wapo wanawake waliokusanya mbegu hizo kutoka kwa waume zao huku wakiwalazimisha waume zao kutumia kondomu ili waweze kukusanya mbegu na kuziuza.

Mwaka 2011 habari kama hii iriripotiwa huko Abuja nchini Naijeria kwamba biashara kama hiyo inaendelea. Hali kama hiyo imeripotiwa mwezi wa nane mwaka huu huko Cameroon kwenye gazeti moja kuwa biashara kama hiyo inaendelea.

Gazeti hilo linasema kuwa machangudoa hao wakishafanya tendo hilo na wateja wao hutupa kondomu kwenye kikapu cha taka na mteja akishaondoa hurudia kikapu cha taka na kuchukua mbegu hizo ili kuzitunza vizuri na wengine wamekuwa wakiweka kwenye majokofu ili zitunzike vizuri.

Huko Camerron kuna machangudoa wamekiri kukusanya mbegu hizo na kuzipeleka kwa waganga wakizifanyia mambo ya kishirikina.

Sijajua hapa Dar es Salaam hali ikoje.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW