DStv Inogilee!

Machinjio yaliyokutwa na ‘mizoga’ ya ng’ombe yafungiwa

Siku kadhaa baada ya kukutwa kwa mizoga ya ng’ombe katika machinjio ya Tegeta jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameifungia machinjio hiyo kwa muda usiojulikana huku mmiliki wake akisakwa.

Akizungumza Bungeni mjini Dodoma, Mpina amesema kuwa wananchi wasiwe na mashaka na mtu yoyote na nyama ya Tanzania ni bora na inatoka kwenye malisho bora.

“Vyombo vyetu kwa maana ya Mkurugenzi wa Mifugo, Bodi ya Nyama, TFDA na Halmashauri tunao usimamizi mathubuti katika mabucha yetu katika machinjio zetu katika kuwahakikishia usalama walaji na kwa pointi hiyo nataka niweke wazi kwa walaji, wananchi wote wasipewe mashaka na mtu yoyote nyama za Tanzania ni bora na nyama za Tanzania zinatokana na malisho bora na kwamba wasipewe hofu kwamba Watanzania wanaweza wakala vibudu,” amesema Mpina.

Hata hivyo, Mpina ameongeza kuwa huyo mwenye machinjio aliyekuwa anafanya jaribio tu tayari amefungiwa machinjio yake.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW