Soka saa 24!

Machozi Bendi yatimiza miaka sita

Machozi_6_face
BENDI  ya machozi juzi ilikuwa ikisherekea Barthday kwa kutimiza miaka sita tangu kuanzisha kwake mwaka 2005, katika sherehe hiyo iliyokuwa ikiambatana na kukata keki na kutoa tuzo kwa wasanii na wadau wake ilifanyika katika Raustarant yao ya  Nyumbani Loudge.

Kiongozi wa bendi hiyo mwanamuziki  Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jay dee’, pamoja na mumewe Gadner G Habash, wanasema kwa pamoja wanatoa shukurani kwa wapenzi wa bendi hiyo kutokana na  kushirikiana kwa pamoja siku zote.

Judith pia alitoa wasaa na shukrani zake kwa wanamuziki wa bendi hiyo hususani wa kiume, ambao siku zote wamekuwa naye pamoja ni tofauti sana na wasanii wa kike ambao hadi sasa hana hata mmoja baada ya kukaa kwa muda na kuondoka.

Jide pia aliwashukuru wadau wa bendi hiyo ambao wamekuwa nao pamoja tangu kuanzishwa kwa bendi hiyo, ambayo ilianza kama utani na kuhamia sehemu mbalimbali na hatmaye kurudi nyumbani Loudge.

Pia hakuacha kueleza kwamba kufika pale ni kutokana na uvumilivu mkubwa alionyesha , kwani hakuna kazi iliyokosa matatizo.

Machozi_6_keki
Keki ya Machozi Bendi, ambayo iliandaliwa kwa mafano wa Mixture  ya muziki.
Machozi_6_Gadner
Katika masuala ya kukata keki na kulishana, ilifika mpaka zamu ya Captain Gadner
Machozi_6_jamaa
Mwanamuziki wa Machozi bendi, ambaye alipata tuzo ya msanii anayevaa vizuri
Machozi_6_judithi_pombe
Hata ilikuwa zamu ya kugonga Cheez, kwaajili ya kubariki bendi ya kusherekea kwa kutimiza miaka sita
Machozi_6_Mandojo_Domo_kaya
Man dojo na Domo kaya nao walikuwepo na kupata kitu cha keki.
Machozi_6_Sam_keki
Ikafika zamu hadi ya wasanii pia wakapata keki, huyu ni Sam wa Machozi bendi
Machozi_6_waimbaji
Baada ya keki ikafika  zamu ya kudondosha mojamoja kwenye buludani
Machozi_6_wanacheza
Hatmaye ikawa hivi………
Machozi_6_kiayo
Lakini baadaye ikaja kuwa miyayo kwa wengine…………. Sijui usingizi au njaaa

By Mo ‘ones

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW