Burudani

Machozi yaandaa Party ya miaka 6

Machzo_Bandi_wakitumbuiza

BENDI ya machozi inayooongozwa na mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ au Binti Machozi  inatarajia kufanya Party, kwaajili ya kujipongeza kwa kutimiza miaka sita ya bendi hiyo. Akiongea meneja wa bendi hiyo na mume wa mwanamuziki Lady Jay Dee,  Gadner G Habash amesema Party hiyo watatoa tuzo za pongezi kwa wale wadau wa machozi wa muda mrefu.

Gadner amesema watu hao ambao wamejitolea kwa shida na raha tangu bendi hiyo ilipoanzishwa, na hawajawahi kuwaacha hata siku moja kwa ushauri na misaada midogo midogo kwao ni watu muhimu sana.  Aidha alidai kwamba kwenye Party hiyo, watatandika kapeti jekundu kwaajili ya kuonyesha heshima hiyo, kwakuwa ni watu muhimu sana.  Pia aliongeza kwa kusema  watu mashuhuri watakaribishwa kwenye Party hiyo, ambayo Machozi yenyewe itatoa burudani.

Miongoni mwa wakari wa bendi hiyo, ni Rapper  Mau Santiago, mkari wa Bss Bella, mtaalam wa sauti Sam, mkari wa sauti na  mtalaama wa  RnB Tanzania Stive RnB wakati kiongozi wa mashambulizi hayo yote ni mwanadada Komando Lady Jay Dee na  wengine.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents