Habari

Madaktari 381 kutoka China kutibu bure wakazi wa Dar ndani ya meli (Video)

Madaktari Bingwa na wataalamu wa afya 381 kutoka Jeshi la China wanatarajiwa kuwasili kwa meli katika bandari ya Dar es salaam tarehe 19 Novemba 2017 kwa ajili ya kufanya matibabu bure kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika kuwahudumia wananchi.

Inakumbukwa mwaka huu wakati wa zoezi la matibabu ya bure yanaendelea jijini Dar es salaam aliyekuwa balozi wa Tanzania kutoka China aliahidi kushilikiana na Tanzania  katika nyanja za afya ahadi ambayo imezaa matunda ambapo kuanzia tarehe 19 mwaka huu timu ya madaktari 300 watatoa huduma za matibabu bure.

RC Makonda amesema madaktari hao watahudumia wananchi 600 kwa siku ndani ya meli hiyo ambapo matibabu ya kawaida pamoja na upasuaji utafanyika bure na kuwataka wakazi wa DSM na mikoa jirani kutumia vyema fursa hiyo itakayodumu kwa siku 7.

Mkuu huyo alisema atatangaza utaratibu mpya wa matibabu hayo ili kuwe na mtiririko ambao utawafanya watanzania kutibiwa kwa urahisi zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents