Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Madaktari bingwa wa moyo watua nchini, 50 kufanyiwa upasuaji (Video)

Taasisi isiyo ya kiserikali ya International Islamic Relief Organization of Saudi Arabia (IIROSA) imewaleta nchini Tanzania madaktari Bingwa wa Moyo kwaajli ya kuwafanyia upasuaji wa moyo watanzania 50 kupitia Taasisi ya Moyo ya JK Kikwete.

Akizungumza na waandishi, Mr. Ahmed Farid ambaye ni msimamizi wa zoezi hilo nchini Tanzania akiwapokea madaktari hao kutoka nchini Saudi, alisema zoezi hilo litaanza kufanyika kuanzia kesho.

“Tunawashukuru sana International Islamic Relief Organization of Saudi Arabia (IIROSA) kwa hili jambo, ni jambo la heri sana kwetu na tayari tumeshawaandaa wagonjwa hao 50 ambayo watafanyiwa upasuaji,” alisema Farid.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW