Habari

Madaktari wamuokoa mkulima aliyechomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni

Kuna msemo usemao hakuna aijuae kesho yake, huku wengine husema kesho ni fumbo hii imetokea mjini Morogoro kwa mkulima na mkazi wa kijiji cha Dodoma Isanga kata ya Masanze wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Augustino Mtitu aliyechomwa mkuki mdomoni na hatimaye mkuki huo kutokea shingoni.

Tukio hilo ni la Desemba 25, mwaka huu, baada ya mtu huyo kujaribu kuzuia vurugu hizo, zilizokuwa zimetokea baada ya wafugaji hao kulisha mifugo yao katika shamba la maharage na mahindi katika kijiji hicho. Umemjeruhi hivyo kulazimika kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, kufanyiwa upasuaji kuondoa mkuki huo na kuokoa maisha yake.

Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Sanifa Mdee, alisema walimpokea mgonjwa huyo akiwa na mkuki mdomoni, ulitokea upande wa shingoni na kuanza kumpatia matibabu na kumtoa mkuki huo, ambapo alilazwa wodi namba moja hospitalini hapo.

Habari njema ni kuwa madaktari wamefanikiwa kuutoa mkuki huo na Mtitu anaendelea vizuri.

Mtitu na wengine wanane walijeruhiwa katika vurugu zilizohusisha jamii ya wafugaji wa Kimasai na wakulima wa kijiji hicho kilichopo wilayani Kilosa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema mpaka jana watu watatu walikuwa wanashikiliwa na Polisi, na msako unaendelea kuwasaka wale wote waliohusika katika kufanya vurugu hizo.

Kutokana na tukio hilo, wananchi wenzake waliamua kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa ajili ya matibabu. Baadae alihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji na matibabu zaidi ya kuokoa maisha yake.

Baada ya kutokea kwa tukio hilo, muda mfupi baadaye wafugaji hao walirudi tena kijijini hapo, kwa lengo la kuokoa mifugo yao iliyokuwa imekamatwa, na ndipo walipoanzisha tena vurugu kwa kuwashambulia watu wengi wanane akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji pamoja na wa Kitongoji.

Watu watano, kati ya waliojeruhiwa, walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kupatiwa matibabu. Diwani wa Kata ya Masanze, Bakari Pilo, akizungumza kwa njia ya simu, alisema hilo ni tukio la tatu kutokea kwenye kata yake katika kipindi kifupi.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents